Wednesday, 30 April 2008

WANAFUNZI WA MUM WAKIWA MJINI DODOMA


Uongozi wa serkali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha waislamu Morogoro wakiwa mjini Dododma kwa ziara fupi ya kujifunza uongozi.

MAMBO YA MJENGO MJINI DODOMA


Hapa ni mjini Dodoma ambapo mjengo au BUNGE letu lipo hapo.

MAZINGIRA MAZURI.


Mazingira mazuri ambayo yamo katika chuo kikuu cha waislamu mjini morogoro

KUSOMA KWA PROJECTA


Wanafunzi wa MASS COMMUNICATION mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro wakiwa katika lecturer kwa kutumia projector.

Friday, 25 April 2008

BONANZA LA VYUO VIKUU MJINI MOROGORO


Mchezaji wa Chuo Kikuu cha Mzumbe akijivinjari katika mchezo wa baskatball kwenye bonanza la vyuo vikuu mjini Morogoro.

BONANZA LA VYUO VIKUU MJINI MOROGORO


Umati wa watu waliokusanyika kuangalia bonanza la vyuo vikuu mjini morogoro.

BONANZA LA VYUO VIKUU MJINI MOROGORO


Pichani Mzumbe University wakipambana vikali na Muslim University katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro..

SHANGWE ZA BONANZA MJINI MROGORO.


Mashabiki hao kutoka Muslim Univrsity of Morogoro wakiwa na furaha baada ya timu yao ya volley bal kuibuka mshindi jana katika Bonanza la Vyuo vikuu mjini Morogoro.

BONANZA LA VYUO VIKUU MJINI MOROGORO


Pichani mchezaji kutoka Chuo Kikuu cha Muslim University of Morogoro akiuwahi mpira katika pambano lilifonyika mjini Morogoro katika bonanzna la Vyuo vikuu vya mjini Morogoro.

BONANZA LA VYUO VIKUU MJINI MOROGORO


Wachezaji wa basket ball kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiwa nje kwa mapumziko mafupi.

BONANZA LA VYUO VIKUU MJINI MOROGORO


Pichani ni wachezaji wa timu ya Chuo Kikuu cha Muslim University of Morogoro wakiwa wanapewa mawaidha ya mwisho kabla ya kuanza ngwe ya pili ya lala salama.

BONANZA LA VYUO VIKUU MJINI MOROGORO


Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiwa kwenye Bonanza la vyuo vikuu mjini Morogoro jana. Huyo mwenye t shirt nyekundu ni mchezaji hatari sana wa timu ya Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Tuesday, 15 April 2008

UMATI WA WANAWAKE WAKIWA KWENYE SHEREHE ZA MWAKA NCHINI SWAZILAND.

Kama wanavyoonekana umati mkubwa wa wanawake wakiwa kwenye sherehe zao za kila mwaka. picha kwa hisani ya SHEIKH MPEKA

WAZAZI WAKIWA NA MTOT WAO MWENYE ULEMAVU


Wazazi wa mtoto wa ajabu wakiwa na mtoto wao nje ya hospitali ya taifa nchini Jamaica pamoja na watoto wao wengine.

WANAWAKE WA SWAZILAND WAKIWA KWENYE UTAMADUNI WAO.


Wanawake wa Swaziland wakiwa kwenye sherehe zao za kila mwaka baada ya hapo mfalme wa nchi hiyo huchagua mmoja miongoni mwao kuwa mkewe.

MAAJABU YA DUNIA HAYA JAMANI.....


Mtoto wa ajabu amezaliwa huko Jamaica kama anavyoonekana kwenye picha, madactari bingwa wameshindwa kumfanyia upasuaji..

Monday, 14 April 2008

MWALIMU MTARAJIWA


Mwalimu mtarajiwa akijiandaa katika kazi yake ya ualimu, mwalimu huyu anajulikana kwa jina la DOI.Lakini mara nyingi kazi ya ualimu ni wito.

KARIBU MJINI MOROGORO


Hapa ni mjini Morogoro karibu kabisa na round about.

ROCK CITY KWENYE PICHA.


Hapa mjini Mwanza karibu kabisa na ziwa victoria, mji huu umepewa jina na hupendelewa kuitwa THE ROCK CITY.

MAMBA NI WANYAMA HATARI SANA.


Hapa mamba wakiwa kwenye zizi lao, picha hii ni kwa hisani ya sheikh JOKA.

HILI SI GOGO NI JOKA KUBWA AINA YA CHATU


Hapa ni joka kubwa likikatiza katikati ya barabara karibu kabisa na kijiji cha Matombo.

TIMU YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)


Hii ni timu ya Chuo Kikuu cha Dodoma,kama ilivyopigwa picha na msamaria mwema wetu.

MITAA YA MJI WA MOROGORO


Hii ni sehemu ya mji wa Morogoro ambako siku hata siku kunazidi kupendeza, hii ni kutokana kukua kwa miji mingi sehemu baerani africa hata kwetu Tanzania.

KIJIWE STORI ZAMANI KIJIWE MAHABA..

Vijana hao walikutwa wamekaa kijiweni hapo, zamani kijiwe hiki kilijulikana na kuitwa kijiwe MAHABA lakini sikuhizi kinaitwa kijiwe fikra au kijiwe stori. Picha kwa hisani ya SHEIKH MKUNDWA

HIZI SUTI SI ZA KITOTO

Kijana huyo ametinga SUTI zile za akina wakoloni, kipindi hicho SUTI hizi zilikuwa hazinunuliki kwa watu wa kawaida walikuwa wanavaa wazungu tuuu.

MJINI MOROGORO KUMEKUCHA

Hapa ni katikati ya manispaa ya Mjini Morogoro ambako ni karibu kabisa na kituo cha daladala za ndani ya mji wa Morogoro. Shughuli mbalimbali zinafanyika hapa.

KIKOSI CHA MUM KILICHOTINGA MJINI DODOMA

Hiki ndicho kikosi cha wana MUM kilichotinga mjini Dodoma na kutandikwa goli kadhaa japo sio nyingi. Goli hizo zililipwa kwa kuitandika SALVATORIAN bila huruma

TUZINGATIE HAKI ZA WANYAMA

Hapa ni katika kijiji cha KIBAIGWA karibu kabisa na mkoa wa Dodoma kijana huyo akiuza kuku kwa njia hiyo ya kumuinamisha kuku juu chini, hii ni unyanysaji kwa wanyama.

Monday, 7 April 2008

SHEIKH JIBA AKITOA MAWAIDHA MJINI DODOMA JANA

Hapa sheikh JIBA kutoka CHUO KIKUU CHA WAISLAMU MOROGORO akisisitiza jambo mjini Dodoma jana.

CHUO KIKUU CHA DODOMA

Hapa ni cho Kikiuu Cha Dodoma, jana wanafunzi wa Muslim University of Morogoro walitembelea chuoni hapo.

Saturday, 5 April 2008

NUNUA KWANGU JAMANI...............

Wafanyabiashara wa matunda na bidhaa nyingine ndogondogo wakihaha kuuza bidhaa zao kwenye basi ambalo limesimama katika kituo cha mabasi cha Morogoro yaani Msamvu.

SOKO HALINA WANUNUZI MEZA NYEUPEEEEEEE.

Sehemu ambayo wafanyabiashara wadogo wadogo huendesha shughulin zao za kila siku mjini Morogoro likiwa tupu kabisa hamna wanunuzi na meza nyeupe. Eneo hili hujulikana kwa jina la sabasaba.

VIBAKA WAKIDHIBITIWA NA WANA USALAMA

Polisi wakiwadhibiti vijana watatu waliotaka kumpora mwana mama mmoja pochi lake leo mchana mjini Morogoro, pembeni watu wakiangalia tukio hilo.

KARAHA YA MATOPE

Hapa ni karibu kabisa na soko kuu la Mkoani Morogoro, soko hili limezingirwa na matope ambayo huwakera wapita njia hasa wanaotembea kwa miguu.

ATHARI YA MVUA MOROGORO.

Mvua inayoendelea kunyesha nchini kote imeleta athari kubwa katika nchi kwani sehemu nyingine zimeathirika sana. Hapa ni mkoani Morogoro maji yakipita kwa kasi kwenye mtaro.